News
Posted On: Oct 10, 2026
Wagombea Walioidhinishwa Na Bodi Ya Wadhamini Na Kuanza Kwa Kampeni
Ndugu Wanachama, Kamati ya Uchaguzi inapenda kuwataarifu wanachama wote wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kuwa imepokea taarifa kutoka kwa Bodi ya Wadhamini kuhusu uamuzi wa kikao chake kilichofanyika tarehe 10 Oktoba 2026. Katika kikao hicho, Bodi ya Wadhamini imeidhinisha majina yote ya wagombea waliowasilishwa na Kamati, kugombea nafasi walizoomba katika Uchaguzi Mkuu wa TAA utakaofanyika tarehe 17 Oktoba 2026.
WAGOMBEA WALIOIDHINISHWA
Wagombea walioidhinishwa kugombea nafasi mbalimbali ni kama ifuatavyo:
| Na. | Jina la Mgombea | Nafasi |
|---|---|---|
| 1 | CPA Victorius P. Kamuntu (M/580) | Rais |
| 2 | CPA Rejea N. Matata (M/616) | Makamu wa Rais |
| 3 | CPA Amina R. Haghai (M/1021) | Makamu wa Rais |
| 4 | CPA Mfaume Mbuma (M/1002) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 5 | CPA Mkufaya H. Matope (M/749) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 6 | CPA Hyasinter Tarimo (M/2373) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 7 | CPA Moses Kambenga (M/2761) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 8 | CPA Joram Yona Msawa (M/901) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 9 | CPA Frank C. Laurent (M/1024) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 10 | CPA Allen Godwin Moove (M/413) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 11 | CPA Honest Christofa Humba (M/2752) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 12 | CPA Richard Kisika (M/2301) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 13 | CPA Miriam Laizer (M/1193) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 14 | CPA Nipa Neeeema Materu (M/913) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 15 | CPA Chrisant Revocatus Buzalle (M/2074) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
| 16 | CPA Salum Mohamed Mw andu (M/1115) | Wajumbe wa Baraza la Uongozi |
2. KUANZA KWA KAMPENI
Kampeni zinaanza rasmi kuanzia tarehe ya Tangazo hili. Kamati inawakumbusha wagombea wote na wanachama wanaowaunga mkono kuwa kampeni zifanyike kwa ustaarabu, kwa heshima na kwa kuzingatia maadili ya Taaluma ya Uhasibu. Kampeni ziwe za kunadi sera na uwezo wa mgombea, bila kumdhalilisha au kumtolea lugha chafu mgombea yeyote, na zisivuruge umoja wa Chama.
3. NAFASI YA KUJIELEZA SIKU YA MKUTANO MKUU
Wagombea wote watapata nafasi ya kujieleza kwa wanachama siku ya Mkutano Mkuu, tarehe 17 Oktoba 2026, kabla ya kupigiwa kura. Wanachama mnaombwa kuwasikiliza wagombea kwa makini ili mpige kura kwa kuzingatia sifa na uwezo wao. 4. PONGEZI
Kamati ya Uchaguzi inawapongeza wagombea wote kwa kuidhinishwa kugombea, na kwa moyo wa kujitolea walioonyesha katika kukiongoza Chama. Aidha, Kamati inawashukuru wanachama wote kwa ushirikiano wao katika mchakato huu, na inawahimiza kushiriki kwa wingi katika Mkutano Mkuu na kupiga kura.
Tunawatakia wagombea wote kila la heri.
CPA Adv. Emmanuel L. Kalibashubao
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi - Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA)
