Matokeo Ya Uchaguzi Mkuu Wa TAA (2026–2029)

Posted: Oct 10, 2026


MATOKEOYAUCHAGUZA202618OCT.pdf

Date: Oct 10, 2026

Ndugu Wanachama,
Kamati ya Uchaguzi inapenda kuwataarifu kuwa Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 17 Oktoba 2026 umekamilika. Wanachama 1,565 walikuwa na haki ya kupiga kura, na wanachama 132 walipiga kura (asilimia 8.4). Kura zote 132 zilihakikiwa.
Matokeo ni kama ifuatavyo:
1. Nafasi ya Rais

Mgombea Kura Asilimia
CPA Victorius Philbert Kamuntu (mshindi) 118 89.4%
Kura zilizochawa wazi 14 10.6%

CPA Victorius Philbert Kamuntu ameshinda nafasi ya Rais baada ya kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa.
2. Nafasi ya Makamu wa Rais
Mgombea Kura Asilimia
CPA Amina Ramadhani Haighai (mshindi) 91 68.9%
Rejea Nehemia Matata 34 25.8%
Kura zilizochawa wazi 7 5.3%

CPA Amina Ramadhani Haighai ameshinda nafasi ya Makamu wa Rais.
3. Wajumbe wa Baraza la Uongozi (nafasi 15)
Wagombea 13 waliojitokeza wamechaguliwa kama ifuatavyo:
Na. Jina la Mjumbe Kura
1 Nipaneema Cuthbert Materu 98
2 Joram Yona Msawa 93
3 Salum Mohamed Mwandu 93
4 Miriam Ephraim Laizer 91
5 Chrisant R. Buz a ile 90
6 Moses Cleofas Kambenga 88
7 Frank Cyprian Laurent 84
8 Hyasinter Ndewingia Tarimo 83
9 Mfaume Juma Mbuma 77
10 Allen Moova 76
11 Honest Christofa Humba 73
12 Richard Mgendi Kisika 71
13 Mkufya Hassan Matope 68

Kwa kuwa wagombea waliojitokeza walikuwa 13 kwa nafasi 15, nafasi mbili (2) za Wajumbe wa Baraza la Uongozi bado hazijajazwa. Utaratibu wa kuzijaza utatangazwa baadaye kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uchaguzi.
Kamati ya Uchaguzi inawapongeza washindi wote kwa kuaminiwa na wanachama. Inawashukuru wagombea wote kwa ustaarabu na moyo wa kujitolea walioonyesha wakati wa kampeni, na wanachama waliojitokeza kupiga kura. Tunawasihi wanachama wote kuwaunga mkono viongozi wapya ili kulijenga Chama chetu..