Kuandaa Mustakabali wa Uchumi wa Tanzania kupitia Sera za Kifedha
Picha ya pamoja kutoka katika Mafunzo ya Kutoa Mapendekezo kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, yaliyofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa Corridor Springs kuanzia tarehe 28–30 Januari 2026.
Mafunzo hayo yalibeba kaulimbiu:
“Kutumia Sera za Kifedha Kukuza Maendeleo ya Biashara Tanzania ifikapo Mwaka 2050.”
Pichani ni Mgeni rasmi, Mhasibu Mkuu wa Serikali Mhe. CPA Leonard Mkude ( wa tatu kutoka kushoto), Rais wa TAA CPA Godvictor Lyimo (wa pili kutoka kulia), Makamo wa Rais wa TAA CPA Victorius kamuntu ( wa tatu kutoka kulia), Mtendaji Mkuu wa TAA Bi. Winifrida Ngaraguza (Wa pili kutoka kushoto), mwakilishi kutoka CIMA Mr. Miley Rahman (Wa nne kutoka kushoto), pamoja na wajumbe wa Baraza la Uongozi la TAA.
Ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano, kuongeza uelewa wa sera za kifedha na kuchangia mijadala yenye tija kuhusu maendeleo ya biashara na uchumi wa Tanzania..
Avagroup - Indulging a different taste.